
Ajali ya ndege ya ukraine: iran yakana madai kuwa ilidungua ndege ya ukraine - bbc news swahili
Play all audios:

AJALI YA NDEGE YA UKRAINE: IRAN YAKANA MADAI KUWA ILIDUNGUA NDEGE YA UKRAINE 9 Januari 2020 Imeboreshwa 10 Januari 2020 IRAN KWA MARA NYINGINE IMAKANA MADAI KUWA MAKOMBORA YAKE YALIIDUNGUA
NDEGE YA ABIRIA YA UKRAINE KARIBU NA MJI MKUU WA NCHI HIYO, TEHRAN SIKU YA JUMATANO. Mkuu wa mamlaka ya anga amesema ana ''uhakika'' kuwa ndege hiyo haikushambuliwa na
kombora. Mkuu huyo alikuwa akijibu madai yaliyotolewa na viongozi wa nchi za Magharibi kuwa ndege hiyo ilidunguliwa na makombora ya Iran kimakosa. Ushahidi unaashiria kuwa kombora la Iran
lilidungua ndege ya abiria ya Ukrain iliyoanguka karibu na Tehran, kimakosa, viongozi wa magharibi wanasema. Viongozi wa Canada na Uingereza wanataka uchunguzi wa kina ufanyike kubaini
chanzo halisi kilichosababisha, ajali iliyowaua watu wote 176 waliokuwa ndani ya ndege hiyo. Skip Iliyosomwa zaidi and continue reading ILIYOSOMWA ZAIDI * Tetesi za soka Ulaya Jumamosi: Al
Hilal wanakaribia kutoa ofa ya pauni milioni 100 kwa Fernandes * Presha 6 zinazoikabili Simba SC dhidi ya Berkane Zanzibar * 'Wanaume hawana hisia" na habari zingine potofu ambazo
hatuelewi kuhusu "uanaume' * 'Ngome 12 za siri': Jinsi CIA inavyoisaidia Ukraine kupambana na Putin - NYT End of Iliyosomwa zaidi Ukraine awali ilisema kuwa inachunguza
endapo ndege yake iliangushwa na kombora, jambo ambalo mamlaka za Iran zilikanusha vikali. * Ndege ya Ukraine iliyoanguka Iran ilitaka kusitisha safari * 176 wafariki katika ajali ya ndege
Iran Kuanguka kwa ndege hiyo kulitokea saa chache baada ya Iran kushambulia kambi za kijeshi za Marekani nchini Iraq kwa makombora ya masafa marefu. Vyombo vya habari vya Marekani
vinaashiria ndege hiyo ilidhani kuwa ndege ya kivita ya Marekani wakati Iran ilipokuwa ikijiandaa kujibu mashambulio dhidi ya Marekani baada ya wao kushambulia vituo vyake vya kijeshi nchini
Iraq kwa makombora. Kituo cha habari cha CBS imevinukuu vyanzo vya kijasusi vya Marekani vinavyodai kuwa picha za satelaiti zinaonesha mwanga wa makombora mawili ambao ulifuatiwa na mwanga
wa mlipuko. Kituo cha habari cha CBS imevinukuu vyanzo vya kijasusi vya Marekani vinavyodai kuwa picha za satelaiti zinaonesha mwanga wa makombora mawili ambao ulifuatiwa na mwanga wa
mlipuko. Kanda ya video iliyopatikana na New York Times ilionenesha jinsi makombora yalivyokuwa yakipita katika anga la Tehran na baadae kulipuka ilipokutana na ndege. Karibu sekunde 10
baadae mlipuko mkubwa ulisikika ardhini. Ndege iliyoshika moto, inaendelea kupaa. Rais wa Marekani Donald Trump siku ya Alhamisi alisema: "nina mashaka" juu ya (kuanguka) kwa
ndege. "Inawezekana kuna mtu amefanya kosa kubwa." Iran imetangaza kutokabidhi kisanduku cheusi cha kuhifadhi taarifa za ndege kwa kampuni ya ndege ya Boeing ama serikali ya
Marekani kwa uchunguzi wa ajali hiyo. Hatua hiyo inatokana na mzozo uliokomaa baina ya Marekani na Iran, hasa baada ya Trump kuagiza shambulio la anga lililomuua Jenerali wa Iran Qasem
Soleimani Januari 3. Chini ya sheria za kimataifa za usafiri wa anga, Iran ina haki ya kuongoza uchunguzi wa ajali hiyo lakini kawaida huwa kampuni iliyotengeneza ndege pia hushirikishwa kwa
karibu. Ndege hiyo ni Boeing 737-800 ambayo imetengenezwa Marekani, nchi ambayo ni hasimu wa Marekani. CBS na Newsweek waliripoti kuwa maafisa wa ujasusi wa Marekani na Iraq wana hakika
kuwa ndege hiyo iliangushwa na makombora ya Iran. CBS wamechapisha taarifa inayodai kuwa mitambo ya rada ya Marekani ilibaini makombora mawili yakirushwa muda mfupi kabla ya ndege hiyo
kulipuka.Kwa upande wa Newsweek wamewanukuu maafisa wa Marekani na Iraq ambao wanaamini ndege hiyo ilidunguliwa na makombora ya Kirusi aina ya Tor M-1 ambayo Nato huyaita Gauntlet. Maafisa
wawili kutoka makao makuu ya jeshi la Marekani wameithibitishia Newsweek kuwa shambulio hilo lilikuwa la bahati mbaya. IRAN IMESEMA NINI? Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga wa Iran Ali
Abedzadeh amesema: " Ndege hiyo ambayo awali ilikuwa ikielekea magharibi baada ya kupaa ilikata kona kulia kutokana na hitilafu ya kiufundi na ilikuwa ikirejea uwanja wa ndege pindi
ilipoanguka." Abedzadeh ameongeza kuwa mashuhuda waliona ndege hiyo "ikiwaka moto" kabla ya kuanguka na kuwa marubani hawakutoa taarifa yoyote ya dharura kabla ya kujaribu
kurudi uwanja wa ndege wa Imam Khomeini. "Ndege kadhaa za ndani na nje zilikuwa zikipaa katika anga la Iran katika usawa wa futi 8,000 (kama ndege ya Ukraine). Hivyo suala la kupigwa na
makombora haliwezi kuwa na ukweli wowote," ameongeza. Afisa huyo amedai kuwa taarifa za awali za uchunguzi zimeshapelekwa Ukraine na Marekani, ambapo ndipo makao makuu ya Boeing.
Taarifa hizo pia zimepelekwa Sweden na Canada ambao pia wamepoteza raia wao.