
Papa hamasisheni utamaduni wa makutano barani amerika kusini! - | vatican news
Play all audios:

Papa Francisko ametoa wito wa kuhamasisha utamaduni wa makutano katika Ujumbe wake aliutumowa kwa washiriki wa Kongamano la Elimu Katoliki Barani Amerika ya Kusini.Ujumbe wake umetiwa sahini
na Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican.Kongamano lilifunguliwa tarehe 8 Januari na litamalizika tarehe 12 Januri 2020. NA SR. ANGELA RWEZAULA – VATICAN Uongozi, mawasiliano na soko,
ndizo mada msingi zinazoongoza Kongamano la 26 la Elimu Katoliki barani Amerika ya Kusini linaloendelea hadi tarehe 12 Januari 2020 na linafanyika huko Santiago ya Chile. Katika Ujumbe wa
Papa Francisko uliotiwa sahini na Kardinali Petro Parolin, Katibu wa Vatican, Papa Francisko anawatia moyo wahusika wote wa shule katoliki ili kutafakari kwa kina juu ya changamoto za
kukabiliana nazo na kuhamasisha katika mantiki ya mada waayojikta nayo katika utamaduni wa dhati wa makutano na hatimaye ili kuweza kufikia kuwa na mapendekezo ya dhati ya matumaini na imani
ya wakati ujao. MISA YA UFUNGUZI:WAFUASI WA BWANA TUNAHITAJI ELIMU Kongamano hili limeandaliwa na Shirikisho la Elimu Katoliki la Amerika ya Kusini ambalo limefunguliwa tarehe 8 kwa Ibada
Takatifu ya Misa iliyoongozwa na Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Chile Askofu Santiago Silva Retamales. Katika mahubiri yake amesema kiini ni Yesu. “Sisi ni wafuasi wa Bwana ambao
tunahitaji elimu na siyo kutaka itikadi ya mawazo yoyote yale, siyo maadili au dogma yoyote ile bali na Mtu ambaye tunahitaji kukutana Naye”. Na zaidi ameongeza Askofu Santiago Silva
Retamales “tunapaswa kujikita kwa undani juu ya mada za Kongamano hili la Injili. CHANGAMOTO MPYA Naye Askofu Óscar Pérez Sayago, Katibu mkuu wa Kongamo la Elimu Katoliki la Amerika ya
Kusini ambaye ni wa Jimbo la Mtakatifu José wa Temuco, wakati wa hotuba yake amekumbusha kuwa utume wa kimisionari katika kiungo hicho ni kutia moyo katika uinjilishaji wa watu wa Amerika
kwa njia ya elimu. “Ni kipindi sasa cha kuwa na maana ya mitazamo mipya, ya changamoto mpya, ya kizazi kipya katika nchi ambazo sisi tunaishi”. Aidha ameongeza kusisitiza kuwa lazima
kuhamasisha uwepo wa uongozi mpya katoliki katika nyanja mbalimbali za maisha ya binadamu. Na kwa njia hiyo ameongeza ni lazima kuwa na mitindo mipya inayoruhusu kubadilishana wema daima
iwezekanavyo na kuweza kuendeleza utambulisho wa ukristo kijamii.