Macron kujadili wimbi la ghasia za kisiwa cha caledonia

Macron kujadili wimbi la ghasia za kisiwa cha caledonia

Play all audios:


Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa anafanya kikao na mawaziri waandamizi mchana huu kujadili wimbi la ghasia linaloshuhudiwa kwenye kisiwa cha bahari ya Pasifiki kilicho chini ya milki ya


Ufaransa cha New Caledonia. Kikao hicho cha dharura cha masuala ya ulinzi na usalama kwa kawaida huwaleta pamoja rais Macron na maafisa kadhaa wa ngazi ya juu wa serikali ikiwemo waziri


mkuu, mawaziri wa ulinzi, uchumi, mambo ya nje na wa ya ndani. Kimeitishwa baada ya mtu mmoja kuuwawa na makumi ya watu ikiwemo maafisa wa polisi kujeruhiwa katika machafuko yanayoendelea


katika kisiwa cha New Caledonia kupinga mageuzi ya katiba yanayoshinikizwa na Ufaransa. Mageuzi hayo ambayo ni lazima yaidhinishwa na bunge la Ufaransa yatawapatia haki ya kupiga kura watu


walioishi kwenye kisiwa hicho kwa angalau miaka 10. Hata hivyo magauezi hayo yanapingwa na kundi linalopigania uhuru wa kisiwa cha Caledonia ambalo linasema yatapunguza nguvu ya jamii ya


wazama katika ngazi za maamuzi. [embedded content]