Trump aifutia kibali cha mafuta venezuela

Trump aifutia kibali cha mafuta venezuela

Play all audios:


Akitangaza uamuzi huo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Truth Social siku ya Jumatano (Februari 26), Rais Donald Trump ameituhumu serikali ya Rais Nicolas Maduro kwa kile alichosema ni


kutokidhi vigezo vya kidemokrasia kwenye uchaguzi wa mwezi Julai na pia kutokuchukuwa hatua za haraka kuwachukuwa wahamiaji wa Venezuela waliopangiwa kufukuzwa Marekani. Soma zaidi: 


Venezuela yawaachia Wamarekani sita baada ya kukutana na mjumbe wa Trump Kibali hicho kilitolewa na utawala wa Rais Joe Biden mwaka 2022 baada ya Maduro kukubali kushirikiana na upinzani


kuelekea uchaguzi wa kidemokrasia. Trump amesema serikali yake inaufuta uamuzi huo mara moja, ambao upinzani unasema uliiwezesha serikali ya Maduro kupata zaidi ya dola bilioni nne.